Mbunge wa jimbo la Mtama
kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Nape Nnauye amefunguka na kudai
kutohusika na kupanga mambo mbali mbali yanayoendelea nchini baada ya
kutuhumiwa kufanya hilo na mmoja wa raia.
Nape Nnauye amefunguka hayo wakati
akijibu moja ya hoja ya mtu aliyemtuhumu yeye kama Mbunge wa CCM na kusema
kiongozi huyo anajua na kuona haki za raia zikivurugwa
"Naamini unaitwa
Kusiluka,nimesoma lawama zako kwangu,una haki ya kulaumu ili upumue, lakini
kuna kikao nimeshiriki kupanga hayo unayonituhumu?! Nadhani kuwa mkweli kwa
nafsi yako tuhuma hizo ni nzito si sawa kuzisema bila kuwa na hakika, sihusiki
na hayo usemayo na nayalaani pia" Alidai Nape Nnauye
Nape Nnauye aliwataka Watanzania kwa
pamoja kuwasha mishumaa ya matumaini na hapo ndipo mtu huyo alipoibuka
mwananchi huyo na kusema kuwa kiongozi huyo yeye anatambua na kujua
kinachoendelea nchini sasa, jambo ambalo Nape Nnauye amelikana na kusema hata
yeye analaani kwa vitendo vinavyoendelea nchini.
SIHUSIKI KWA MAMBO YANAYOENDELEA NCHINI"NAPE
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment