Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Shein amekutana na uongozi wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kusisitiza haja ya kuendeleza umoja na ushirikiano
kati ya Tume hiyo na ya Zanzibar (ZEC) ili Tanzania iendelee kuheshimiwa
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage, Ikulu Zanzibar.
|
Dkt. Shein amesema hayo leo alipokutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa NEC, Ikulu mjini Zanzibar ulipofika kwa ajili ya kujitambulisha ukiongozwa na Jaji Semistocles Kaijage
Mwenyekiti wa Tume hiyo akifuatana
na Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid pamoja
na Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani.
Katika Mazungumzo hayo, Dkt. Shein
aliupongeza uongozi huo kwa kuendeleza umoja na ushirikiano uliopo kati ya
(NEC) na (ZEC) na kusisitiza haja ya kuendelezwa ili kuendelea kuijengea sifa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuendelea kufanya kazi zao kwa ufanisi
mkubwa.
"Ushirikiano wa pamoja
utasaidia kwa kiasi kikubwa kuendeleza majukumu kwa Tume zote mbili hasa
ikizingatiwa kuwa kila upande una uzoefu wake ambapo kwa Zanzibar masuala ya
uchaguzi hasa wa vyama vingi yalianza tokea mwaka 1957 na baadae kuendelea hadi
hivi leo. Nimevutiwa na mafanikio yaliopatikana na Tume kutokana na kutekeleza
majukumu yao. vyema yakiwemo ya kuhakikisha wananchi wanatumia haki yao ya
msingi ya kupiga kura, wanaendesha chaguzi, wanasimamia na hatimae wanatoa
matokeo kwa wakati", amesema
Dkt. Shein.
Rais Dkt. Shein ameendelea kwa
kusema
"Matumaini yangu makubwa kuwa
Mwenyekiti huyo ataendeleza vyema majukumu yake kama alivyofanya Mwenyekiti
aliyekuwa kabla yake Jaji Mstaafu Damiani Lubuva ambaye muda wake wa kushika
wadhifa huo umemaliza kwa kutoa ushirikiano mzuri na NEC sambamba na kutekeleza
vyema majukumu yake".
Pamoja na hayo, Rais Dkt. Shein
amesema kuwepo kwa ofisi za kudumu NEC Zanzibar ni suala la lazima na kuahidi
juhudi za makusudi zitachukuliwa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kutekeleza jambo hilo ili kurahisisha shughuli za tume hiyo.
Kwa upande wake, Jaji Semistocles
Kaijage amempongeza Rais Dkt. Shein kwa kuendelea kuingoza vyema Zanzibar
kutokana na ushindi mkubwa alioupata katika Uchaguzi Mkuu uliopita ambao
umemuwezesha kuendelea kuiongoza Zanzibar kwa kipindi cha pili.
Rais akutana na Tume ya uchaguzi (NEC)
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment