Mahakama ya Mwanzo
wilaya ya Kinondoni imemhukumu msanii 'Shilole' kulipa TSh Milioni 14 kwa kosa
la kuchukua malipo ya show kiasi cha TSh Milioni 3 kutoka kwa Mary Mussa na
kushindwa kufika kwenye show hiyo usiku wa Pasaka mwaka 2017.
Mahakama hiyo imetoa hukumu hiyo leo
Machi 1, 2018 baada ya kumkuta Shilole na hatia ya kutapeli fedha hizo,
kutokana na kushindwa kufika kwenye show husika kama ambavyo walikuwa
wamekubaliana na Mary Mussa jambo ambalo lilisababisha Mary kupata hasara kutokana
na mashabiki kufanya vurugu kwa kutomuona Shilole kwenye show hiyo kama ambavyo
walitangaziwa awali.
Mahakama hiyo pia imempa muda wa
wiki moja msanii huyo kuwa awe ameshalipa fedha hizo kwani kinyume na hapo
mahakama itashikilia mali za msanii huyo.
Msanii Shilole aliambatana na mumeo
Uchebe mahakamani pamoja na wakili wake, ambapo baada ya hukumu hiyo msanii
huyo hakutaka kuongea chochote na waandishi wa habari.
Mahakama yamhukumu Shilole faini ya milioni 14
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment