Rufaa ya
kupinga hukumu ya kifungo cha miezi mitano jela iliyotolewa kwa mbunge wa Mbeya
Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu
Kusini, Emmanuel Masonga imewasilisha Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya.
Akizungumza mmoja
wa mawakili wa Sugu, Faraji Mangula amesema tayari maombi ya rufaa yao
yamepokewa leo mchana na kupewa kumbukumbu namba 29/2018
“Tayari rufaa
yetu imeshapokewa Mahakama Kuu (Mbeya) na tunachosubiri ni kupangiwa
tarehe ya kuanza kusikiliza tu, ila tunachoshukuru watu wa Mahakama hii wapo
vizuri kushughulikia suala hili,” amesema Mangula.
Mbali na
kukataa rufaa hiyo, lakini pia mawakili hao wanakusudia kuomba dhamana kwa
wateja wao ili waweze kuwa nje katika kipindi ambacho wanakuwa
wanasikiliza rufaa yao.
Sugu na
Masonga walihukumiwa baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kutumia lugha ya
fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.
Wawili hao
walitoa kauli hiyo Desemba 30 mwaka jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya
RUFAA YA SUGU NA MASONGA YAFIKA MAHAKAMA KUU
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment