KATIKA KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI UWT WATOA ELIMU KWA KWA WANAWAKE JINSI WANAVYOWEZA KUPATA MIKOPO YA ASILIMIA 5
Mwenyekiti UWT mkoa wa Arusha Yasmini Bachu akiteta
jambo na Bi Mwajuma Salehe mfanyabiashara wa soko la kisongo
|
Mwenyekiti wa umoja wa jumuiya ya wanawake wa chama cha
mapinduzi mkoa wa Arusha Yasmini Bachu akizungumza na akina mama
wafanyabiashara katika soko la Kisongo lililopo kata ya mateves
|
Diwani wa kata ya Mateves Julius Saing”orie akiwa
anamuelekeza jambo mfanyabiashara katika soko la kisongo
|
Mwenyekiti wa uwt mkoa wa Arusha akiwa anaelekeza jambo
akiwa namwenyekiti wa uwt wilaya ya Arusha
|
Mwenyekiti wa umoja wa jumuiya
ya wanawake wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha Yasmini Bachu amefanya ziara
ya kwatembelea akina mama wafanyabiashara katika Soko la Kisongo kata ya
Mateves halmashauri ya Arusha ili kusikiliza changamoto wanazopata hasa upande
biashara zao wanazofanya kuwapa elimu jinsi ya kupata Mikopo ya serikali
inayotolewa na halmashauri.
Lengo kuu la ziara hiyo ni
kusikiliza kero na changamoto za kina kwa mama wafanyabiashara ndogondogo
kabisa masokoni na minadani ,mbogamboga na mama lishe ambao mitaji yao ni
midogo na kuziwasilisha kwa serikalini halmashauri na mamlaka zingine
Akizunguka sokoni Hapo Bachu
amewahoji akina mama wanavyonufaika na mikopo inayotolewa kwenye halmashauri
ambayo imetengwa asilimia tano kwa ajili ya Wanawake ili waweze kunufaika
kibiashara na kujikwamua kiuchumi.
Bachu amesema ni wajibu wa wao
kama viongozi kusimamia na kujua akina mama changamoto wanazopitia kwasababu
mtu akiwa kiongozi ni kama sautiya watuwa hali ya chini.
“Leo
nimekuja hapa soko la kisongo kuwatembelea akina mama na kuangalia ni jinsi
ganmi wananufaika na mikopo kwasababu iko kwa ajili yao asilimia tano na hata
kina mama hawa wakijiunga kwenye vikundi vikundi na kujisajili wanapata mkopo
ambao una riba nafuu sana tofauti na huko mitaani mama anakopa unakuta mwisho
wa siku anashindwa kujiendeleza kwasababu anawaza mkopo lakini akipata asilimia
zile tano anachowaza ni ada ya shilingi 40,000 akikamilisha atakuwa
ameshanufaika”Alisema Bachu Yasmini
Ameongeza kuwa Elfu 40 ni ada kwa ajili ya kusajili kikundi inalipwa halmashauri, riba ya mkopo ni asilimia 10, masharti ya mikopo ni nafuu sana kwani dhamana ni kikundi chenyewe ili mradi watambulike kwa mtendaji wa kijiji/mtaa/kata na afisa maendeleo ya jamii"Alisema
Yasmini amewashauri wanawake hao kujisajili kwenye vikundi vya pamoja na wajisajili kwa mwenyekiti wa kijiji ili wapate fursa ya mikopo ambayo serikali ya awamu ya tano imeamua kusaidia akina mama hao.
Amewataka watembelee na wahoji
kila mara mikopo inapotoka ili asilimia hizo wanufaike nazo kwa kuwa kuna wengi
tayari wameshapata mikopo na wamerejesha na wanajitegemea wenyewe.
Hata hivyo amewataka
madiwani,watumishi wa serikali,wenyeviti kuendelea kutoa elimu kwa akina mama
kwa kuwa kuna wanawake wanahitaji mikopo hiyo lakini bado hawajui ni vipi
wataipata na kutumia fursa.
Kwa upande wa akina mama hao
wafanyabiashara wamesema kuwa sasa wako tayari kujiunga na vikundi ili kuomba
mkopo kwasababu hawakuwa wamepewa elimu kuhusu jinsi ya kupata mikopo kwakuwa
baadhi ya watu walikuwa wanawaelekeza tofauti.
“Kweli
mimi nauza maziwa hapa kisongo lakini sikuwa ninajua kuhusu hiyo mikopo
nilikuwa nasikia tu kwa redio lakini huyu mama alivyofika hapa ametuelewesha
vizuri kumbe unalipa shilingi elfu 40 tu ada ambapo mahali kwingine hakuna hiyo
na kumbe mashariti ya kurudisha riba ni asilimia kumi mimi sisi kama wamama
tutaunda vikundi vyetu”Walisema wamama wafanyabiashara
Pamoja na hayo wanawake hao
wameshukuru sana mwenyekiti huyo kwa kuwa tangu waanze kufanya biashara eneo
hilo hakuna hata kiongozi ambaye aliwahi kufika sokoni hapo ili kuwajulia jinsi
wanavofanya biashara zao pamoja na kupewa elimu ya mikopo.
“Sisi hapa tuna miaka zaidi ya
kumi tunafanya biashara zetu hapa ndogondogo lakini hakuna siku kuna kiongozi
amekuja hapa kutupa elimu kama huyu Mwenyekiti wa sisi wanawake kwanza
tunajivunia sasa mana ni mama mchapa kazi anapenda mafanikio yaw engine sasa
leo tungejulia wapi mambo ya mikopo ya kina mama inayotolewa na Magufuli kweli
abarikiwe sana nasiisi kwakweli tumepata mkombozi na hiyo mikopo ije tu”Alisema
mmoja wa akina mama
KATIKA KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI UWT WATOA ELIMU KWA KWA WANAWAKE JINSI WANAVYOWEZA KUPATA MIKOPO YA ASILIMIA 5
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment