Shughuli katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu zilisimama kwa muda baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme katika
transfoma ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) iliyopo katika eneo la
mahakama hiyo
Trasfoma hiyo imelipuka na kusababisha nyaya
mbili kushika moto na kuzua hofu miongoni mwa watu waliokuwa mahakamani hapo,
kuanza kukimbia hovyo.
Tukio hilo limetokea leo asubuhi Machi 1,
2018 wakati kesi mbalimbali zikiendelea kusikilizwa
Akizungumza Mtendaji wa Mahakama Mkoa wa Dar es Salaam, Gasto Kanyairita amesema baada ya kutokea kwa mlipuko huo ulizuka moto na kushika nyaya mbili, ikiwemo ya intaneti ambazo hutumiwa kwa ajili ya mawasiliano ya simu
"Moto uliingia moja kwa moja katika
jengo letu na kushika seva yetu ambayo tunatumia kwa ajili ya mawasiliano ya
simu,” amesema
"Baada ya kushika nyaya hizo,
moto huo uliambaa amba na kuingia katika chumba cha Tehama na kisha kushika
soketi ya umeme iliyopo ndani ya jengo la mahakama.”
Baada ya kutokea kwa hitilafu hiyo ya
umeme, askari polisi walikuwepo mahakamani hapo, alitumia vidhibiti
moto na kufanikiwa kuuzima.
Dakika tano, baada ya kutokea kwa hitilafu
hiyo, gari la zimamoto lilifika mahakamani hapo na kukuta tayari moto huo
umezimwa.
Breaking News:Mahakama ya Kisutu kumetokea Mlipuko
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment