Mchezaji wa Zamani wa
timu ya Simba SC na timu ya Taifa ya Tanzania, Arthur Mambeta amefariki dunia
baada ya kuugua kwa kipindi kirefu jijini Dar es Salaam.
Kutoka na taarifa hizo, Afisa habari
wa Simba Haji Manara amesema wamepokea ujumbe huo kwa mshtuko mkubwa kifo cha
mchezaji huyo ambapo msiba wake unafanyikia Kigamboni.
"Tumepokea kwa mshtuko mkubwa
kifo cha mchezaji wa zamani wa kimataifa wa klabu yetu ya Simba Arthur Mambeta
ambae amefariki jana hapa jijini. Mambeta anakumbukwa sana na wanasimba pale
alipotoka kwenye kustaafu soka na kuja kuisaidia klabu yake kuifunga klabu ya
Yanga kwenye mchezo wa fainali Ligi kuu goli 1-0. Hiyo ilikuwa mwaka 1973 huko
nyuma mchezaji huyo alikuwa ni mshambuliaji mahiri kabla ya kuja kucheza
beki", amesema Manara.
Uongozi wa EATV kwa pamoja unawapa
pole wadau wa soka nchini, familia ya marehemu na klabu ya Simba kwa kuondokewa
na mtu muhimu.
Mchezaji wa Simba afariki baada ya kuugua
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment