Siku mbili baada ya kifo cha mwanafunzi na kiongozi wa
wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Meru nchini
Kenya Evans Njoroge kimefungwa kwa muda
usiojulikana.
Katika taarifa iliyotumwa
kwenye vyombo vya habari nchini humo, Katibu
wa Baraza la Mawaziri Amina Mohamed, ameeleza kuwa ameunda timu
ambayo itafanya uchunguzi wa kutafuta sababu ya kifo cha mwanafunzi huyo.
Inaelezwa kuwa mwanafunzi huyo
aliuawa kwa kupigwa na risasi na polisi siku ya Jumanne February
26, 2018 wakati wa maandamano ya wanafunzi ambayo yalisababisha
vurugu kubwa.
Marehemu Evans alipigwa
risasi na askari wakati akiongoza maandamano hayo ambayo yalikuwa yakipinga
kile walichodai ni kunyanyaswa na Makamu Mkuu wa
chuo hicho huku wakishinikiza ajiuzulu haraka.
Kinachoendelea baada ya mwanafunzi kuuawa kwa risasi na polisi Kenya
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment