Makamu Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kwa pamoja
kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano ili waweze
kuifikisha nchi katika uchumi wa kati.
Mama Samia ametoa kauli hiyo wakati
alipokuwa akitoa salamu zake katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani leo
Machi 8, 2018 ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema kuelekea uchumi wa viwanda
tuimarishe usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake vijijini.
"Tuimalishe sasa maendeleo ya
wanawake kushuka kule vijijini, tuwaibue wa vijijini na wenyewe waweze kujua ni
jambo gani linaendelea ili watoe mchango wao katika kuelekea Tanzania ya
viwanda. Katika kuandimisha siku hii ya wanawake duniani, ninawaombe kwa
dhati kabisa muunge mkono serikali katika jitihada zote ambazo tunafanya", amesema Mama Samia.
Pamoja na hayo, Mama Samia
ameendelea kwa kusema "kila mmoja pale alipo aunge mkono
serikali ili azma tuliyoikusudia iweze kutimia na sote kwa pamoja tuingie
kwenye maendeleo ya viwanda na tuipeleke nchi yetu kwenye uchumi wa kati pale
itakapofika 2025".
Kwa upande mwingine, Makamu wa Rais
amesema mpaka sasa jitihada serikali ya Tanzania imefanya katika kuhakikisha
inamuinua mwanamke na itaendelea kufanya hivyo siku zote.
UJUMBE WA MAMA SAMIA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 08, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 08, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment