Jeshi la Polisi Mkoani
Iringa limefunguka na kuweka wazi kuwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu UDSM, Adbul
Nondo alifika kituo hicho cha polisi jana Machi 7, 2018 na kusema kuwa alitekwa
na watu wasiojulikana.
RPC mkoa wa Iringa, Juma Bwire
amesema kuwa jeshi la polisi limefungua jalada la uchunguzi ili kubaini ukweli
kama mwanafunzi huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania
kama kweli alitekwa au la.
"Jeshi la polisi mkoa wa Iringa
limefungua jalada la uchunguzi kubaini ukweli kama alikuwa ametekwa na kama
alitekwa tunaaidi kwamba sisi jeshi la polisi likiwapata watuhumiwa sheria
itachukua mkondo wake aidha tunaendelea kuchunguza kama ametoa taarifa za uongo
kwa njia ovu kwa lengo la kutaka kuhamasisha wanafunzi wenzake ili kuleta
uvunjifu wa amani nchini tutamshughulikia kama waalifu wengine"
Aidha RPC amesema kuwa mwanafunzi
huyo kwa sasa anaendelea vizuri na wala hana majeraha yoyote yale kwani
hajapigwa na ni mzima wa afya njema na kusema jeshi la polisi linaendelea na
uchunguzi wa tukio hilo ili kujua nini kilimsibu.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi
Tanzania Abdul Nondo alipotea katika mazingira ya kutatanisha Machi 6, 2018
akiwa jijini Dar es Salaam majira ya saa tano usiku na kupatikana Mafinga
Iringa Machi 7, 2018.
Nondo Hana majeraha yoyote- Polisi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 08, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 08, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment