Mbunge wa Nzega (CCM),
Hussein Bashe amewahakikishia wananchi wa Tanzania kuwa hoja yake
aliyoiwakilisha kwa Katibu wa Bunge kuwa haiwezi kukwamishwa na jambo lolote
kwa madai hakuna kisichojulikana kinachoendelea kutoka katika nchi.
Bashe ametoa kauli hiyo leo (Machi
08, 2018) wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es
Salaam kwa lengo la kuelezea sababu zilizompelekea yeye kama Mbunge kuandika
barua ya kutaka kuundwe kwa kamati ya uchunguzi dhidi ya matukio mbalimbali
yanayoonesha kutishia umoja, usalama na mshikamano wa taifa la Tanzania.
"Madhumuni ya kikatiba ya Chama
cha Mapinduzi (CCM) ni kuwasemea wananchi, kuwatetea kwa hiyo natimiza
wajibu wangu kama Mbunge sioni kama nitapoteza Ubunge wangu katika hili.
Mimi ninaamini nitapoteza ubunge wangu kwasababu zifuatazo, endapo nitashindwa
kutimiza wajibu wangu ndani ya Bunge, nikishindwa kutimiza wajibu wangu ndani
ya Jimbo langu kwa maana nimeshindwa kuisimamia serikali katika kuleta
maendeleo, nimeshindwa kutimiza ahadi wakati wa uchaguzi katika jimbo langu na
mwisho wanaccm watakaposema kwenye mchakato wa kidemokrasia wa kura kwamba
Hussein wewe hapana", amesema
Bashe
ameendelea kusema
"Mimi ni muumini wa kiislamu
ninaamini kila binadamu umauti utamfika (kifo) na chochote kitakachonifika ni
kile ambacho amekipanga Mwenyezi Mungu lakini sina hofu yeyote kwasababu hili
sio taifa la namna hiyo. Nikiwa kama Hussein sidhani hii hoja kama
inakwenda kukwama kwasababu unapoikwamisha hoja unapaswa kusema unaikwamisha
kwa kutumia misingi gani kama watu wanaamini kwa kila kinachotokea ndani ya
ardhi ya Tanzania sioni kama itakwama".
Pamoja na hayo, Bashe ameendelea kwa
kusema "Bunge limeshafanya maamuzi mbalimbali juu ya masuala
mbalimbali katika rekodi ya nchi hii, kwa hiyo mimi nadhani ni muhimu tukatoa
fursa jambo hili lifike Bungeni na likifika huko kama litakataliwa basi tujue
ni kwasababu zipi na kama nilivyofanya kuwaambia watanzania ndivyo hivyo
nitarudi kuwaambia limekataliwa kwasababu zipi na hapo tutajadili hatua za
kufanya".
Kwa upande mwingine, Bashe amesema
anasubiria majibu ya barua aliyotuma kutoka kwa Katibu wa Bunge Pamoja na
Katibu Chama cha Mapinduzi (CCM) ambayo ameeleza dhamira na nia yake huku
akisisitiza zaidi kuwa jambo hilo hajalifanya kwa mihemuko (kukurupuka) bali
amefanya kwa umakini wa hali ya juu na utafiti wa kutosha.
Chochote kitachonifika amekipanga Mungu - Bashe
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 08, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 08, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment