Zikiwa zimepita siku chache tangu kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ,Charles Mkumbo apate ajali mbaya akitumia gari la Polisi ,askari wengine watatu wa jeshi hilo mkoani Arusha wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari la polisi wakati wakisindikiza fedha za benki kuu.
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo alisema kuwa, ajali hiyo imetokea jana katika barabara ya Arusha Moshi eneo la Tengeru mkoani hapa,majira ya saa 9 :30 Alasiri wakati gari la Polisi likiwa kwenye msafara wakitokea jijini Arusha
Alisema kuwa,gari hilo la polisi lenye namba PT 1715 aina ya Land a cruse lilikuwa likiendeshwa na Askari PC Ismail na alipofika eneo la tukio aligongana na Lori la mchanga aina ya Tipa na kusababisha askari polisi ambaye ndiye dereva kuvunjika miguu yote miwili na kuumia vibaya kichwani.
Kamanda Ilembo alisema kuwa, ajali hiyo ilisababisha pia majeraha kwa askari wengine wawili waliokuwa kwenye gari hilo, ambapo baada ya ajali hiyo dereva wa Lori alikimbia na jeshi la polisi linafanya msako zaidi katika kumtafuta ili achukuliwe hatua
Aidha aliongeza kuwa gari la Polisi limeharibika vibaya kutokana na ajali.hiyo.
Alisema kuwa, askari huyo amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Mount Meru akiwa na hali mbaya na wanafanya taratibu za kumhamishia katika hospital ya rufaa ya Muhimbili jijini Dar es salaam Kwa matibabu zaidi huku majeruhi wengine wawili hali zao zikiendelea vizuri.
Ajali huyo imekuwa wakati jeshi hilo bado likiwa na kumbukumbu ya kamanda wake RPC Mkumbo ambaye bado anauguza majeraha ya ajali iliyotokea eneo la Mdorii Babati wakati akitoka kumsindikiza IGP Siro ,na kumsababishia majeraha mbalimbali ambapo hali yake Kwa sasa inazidi kuimarika.
Mwisho

ASKARI AVUNJIKA MIGUU VOTE BAADA YA KUPATA AJALI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 08, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 08, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment