UDUMAVU WA WATOTO KUWA TISHIO KAGERA


WATOTO 12 walio na umri chini ya miaka mitano kijiji cha Mussenyi, wilayani Biharamulo, mkoani Kagera wamebainika kuwa katika udumavu na hatari ya afya ya ukuaji kutokana na kutokuwa na lishe stahili.

Kauli hiyo ilitolewa na Mratibu wa lishe wilayani humo, Salim Issa, wakati akitoa taarifa ya hali ya maendeleo ya afya za watoto walio chini ya miaka mitano katika mkutano wa ukaguzi wa mashamba darasa ya viazi lishe yaliyoandaliwa na Jukwaa la Biotechnologia nchini (OFAB), kupitia Tume ya Taifa Sayansi na Technolojia (Costech), kwa kushirikiana na serikali ya mkoa huo.

Issa alisema wilaya hiyo ina asilimia 10 ya kutokuwa na lishe ikiwa asilimia 9.2 ya maendeleo ya watoto wapo katika alama ya rangi kijivu na asilimia moja, katika rangi nyekundu kwenye kadi zao za mahudhurio ya kliniki.

Ukiangalia wilaya nzima inahitaji lishe hasa kwa watoto chini ya miaka mitano ndio wenye madhara makubwa ukifuatilia katika kadi za mahudhurio ya kliniki utajionea alama za kijivu na nyekundu na hivi sasa kuna watoto13,790 waliopo kwenye kijivu kwa wilaya nzima, " alisema Issa.

Alisema, baadhi ya kaya hukosa milo inayostahili na kulazimika kutumia aina moja ya chakula ambacho hakijaandaliwa kwa ajili ya mtoto kumsaidia katika hali ya ukuaji

UDUMAVU WA WATOTO KUWA TISHIO KAGERA UDUMAVU WA WATOTO KUWA TISHIO KAGERA Reviewed by KUSAGANEWS on March 21, 2018 Rating: 5

No comments: