Bunge la Zambia
limemsimamisha waziri kwa muda wa mwezi mmoja asihudhurie vikao kutokana na
kosa la kumpiga mbunge kwenye viwanja vya Bunge.
Spika wa Bunge la Taifa, Patrick
Matibini amesema Waziri wa Jimbo la Lusaka, Bowman Lusambo amesimamishwa baada
ya kumchapa kibao mbunge Chishimba Kambwili hapo Oktoba mwaka jana, na kusema
kwamba tabia hiyo haikubaliki dhidi ya mbunge.
"Hili ni Bunge la heshima, nina
wajibu wa kuhakikisha kwamba heshima na haiba ya Bunge inalindwa na
inahifadhiwa wakati wote," amesema spika huyo.
Kutokana na kusimamishwa huko Waziri
Lusambo hatapata marupurupu na mshahara kama mbunge kwa mwezi wote anaotumikia
adhabu.
Imeelezwa kwamba ni jambo la kawaida
kwa wabunge kutumia lugha isiyofaa na kuleta mizozo, lakini kwa kitendo cha
Waziri kumpiga mbunge hakikuwa cha kuvumilika.
BUNGE LAMSIMAMISHA KAZI WAZIRI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment