Mkongwe wa Muziki wa
Taarabu, Bi Khadija Omary Abdallah Kopa amedai kuwa baada ya kushindwa kupata
Ubunge wa Viti Maalumu kupitia UWT alikata tamaa ya kuendelea kugombea
ingawa ameendelea kuwa mwanachama wa CCM na haoni kwingine pa kwenda.
Hayo ameyasema Bi. Khadija mapema
leo alipokuwa katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia
kurasa za EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa 8:00 mchana hadi 10:00
alasiri.
Khadija amesema kuwa ndani ya CCM
nafasi kubwa aliyowahi kuishika ni kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu CCM kwa muda wa
miaka 10 na kwa sasa hatamani kugombea nafasi nyingine kwa kuwa ndoto zake za
kuwania ubunge zilishakatika tangu aliposhindwa kuingia bungeni miaka
iliyopita.
Mkongwe huyo amefafanua kwamba
hakufikiria kama angekosa nafasi ya kwenda bungeni kwani kipindi hicho alikuwa
akijitahidi kuwa mbele sana katika kufanya kazi za chama lakini uchaguzi
ulipofika wenzake walimpita kwa kuwa walikuwa wana tumia vitu vya thamani
kushawishi huku yeye akiwa hana.
Aidha Bi. Khadija ameongeza kwamba
pamoja na kuwa kwa sasa hana nafasi ya Uongozi CCM hawezi kukihama chama hicho
kwani hapo ndipo alipofika na haoni mahali pengine kwa kwenda.
Khadija Kopa haoni pakwenda zaidi ya CCM
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment