Waziri wa Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi amesema Tanzania inatarajia kupeleka
wataalamu wake wa masuala ya intelijensia nchini Israel kwa ajili ya kupatiwa
mafunzo maalumu.
Dkt. Mwimyi amezungumza hayo leo
(Machi 21, 2018) Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumpokea Waziri wa Ulinzi
wa Taifa ka Israel Avigdor Liberman na kusema wamekubaliana kuhakikisha
wanaimarisha mambo yakiusalama ndani na nje ya nchi hizi mbili na kubadilishana
mbinu mpya za kupambana na wahalifu hata kwa zile njia ambazo ni ngumu kufikia
katika hali ya kawaida.
"Mchango wa Israel katika
teknolojia duniani ni mkubwa sana hivyo ni vyema nchi kuhakikisha wananufaika
nayo katika nyanja zote hasa zile zinazotegemea Tehama kwani nchi hiyo ni moja
ya nchi yenye tekinolojia ya hali ya juu sana duniani hasa kwa mambo ya
kiusalama, ulinzi na mashine mbalimbali zikiwemo zile za matibabu", amesema Dkt. Mwinyi.
Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi wa
Taifa la Israel Avigdor Liberman amesema uhusiano wa nchi hizo mbili ni mkubwa
na wamuda mrefu ndio maana wameamua kuleta tekinolojia za kiusalama ili
kuilinda Tanzania na wahalifu sambamba na hapo wataendelea kutoa ushirikiano
wao kwa ujuzi na ugunduzi wa tekinolojia mbalimbali hasa zinazohusiana na
usalama wa nchi.
Tanzania kupatiwa mafunzo maalum Israel
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment