Jeshi la Polisi Jijini
Dar es Salaam linamshikilia mfanyakazi wa ubalozi wa Syria akihusishwa na tukio
la kushambuliwa, kuibiwa takribani Euro 93,000 Mhasibu wa Ubalozi huo nchini
Tanzania siku ya Jana.
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kinondoni, RPC Muliro Jumanne Muliro wakati alipokuwa
anazungumza na waandishi wa habari leo (Machi 21, 2018) baada ya kupita
takribani siku tatu tokea lilipofanyika tukio la kushambuliwa mhasibu wa
Ubalozi wa Syria kwa kutumia nondo na kufanikiwa kuiba fedha alizokuwa
anazipeleka kuzihifadhi katika moja ya benki na kutoroka na dereva aliyekuwa
anaendesha gari hilo.
"Jeshi la Polisi lilifanya
msako mkali na likafanikiwa kulipata gari alilokuwa akitubia Balozi likiwa
limetelekezwa eneo la Msasani eneo la bonde la Mpunga Jijini Dar es Salaam
ambapo limekutwa limefungwa lakini dereva aliyekua amekula njama na wale
waharifu alikuwa ameshatokomea",amesema
RPC Muliro.
Pamoja na hayo, RPC Muliro
ameendelea kwa kusema "upelelezi juu ya shauri hili
linaendeelea na Polisi wanafanya kila wawezalo kwa kushirikiana na idara
mbalimbali za Jeshi la Polisi kuhakikisha kwamba waharifu wote waliokula njama
wanakamaatwa na hatua za kisheria kuchukuliwa. Kwa kifupi tukio hili
limegubikwa na njama za moja ya mtumishi aliyeajiriwa na ubalozi wa Syria na
hatimaye kufanyakazi na mharifu bila ya kujitambua, mtuhumiwa mmoja
ambaye ametokana na sababu za kiuchunguzi anashikiliwa na Jeshi la Polisi na
nina uhakika atatusaidia kupatikana kwa waharifu wote walitumika katika tukio
hili wanakamatwa".
Kwa upande mwingine, RPC Muliro
ametoa wito kwa mashirika ya umma na yasiyokuwa ya umma kuwa makini pindi
wanapotoa ajira kwa watumishi pindi wanapotaka kuwapa ajira katika maofisi yao
ili kuweza kujikinga na kumuajiri mtu ambaye ni mwizi kwa namna moja ama
nyingine.
MFANYAKAZI WA UBALOZI WA SYRIA ASHIKILIWA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment