Malkia wa muziki wa
Taarab Afrika Mashariki na kati kama anavyojiita mwenyewe, Khadija Omar Kopa,
ameweka wazi juu ya tukio lake alilowahi kufanya wakati yupo kijana la kutoa
mimba, na kwamba anajutia kwa maisha yake yote.
kizungumza kwenye kipindi cha
#KIKAANGONI kinachorushwa kupitia ukurasa wa facebook wa East Africa
Television, Khadija amesema mimba hiyo aliipata akiwa kijana na akiwa kwenye
chati, hivyo akaona itamuharibia mipango na kuamua kutoa, lakini ni jambo analomuomba
Mungu amsamehe kwani si jambo zuri kulifanya.
“Najuta kwweli kweli wakati ule ndio
jina limesimama kweli kweli na mimba wapi na wapi, ukute mwanangu angekuwa rais
sasa, namuomba Mungu anisamehe, najuta sana na vijana msifanye hilo. Mungu
naomba anisamehe sitaki kulisikia tena jambo hilo”, amesema Khadija Kopa.
Khadija Kopa ameendelea kwa kuwataka
mabinti kutofanya jambo hilo na kujiepusha nalo, kwani ni ujinga na siyo kitu
kizuri.
“Kutoa mimba ni ujinga sana, maana
saizi ningekuwa na watoto wangu kama saba, hivyo mabinti zangu nawashauri msije
kutoa mimba kwani ni kitu kibaya sana”, amesema Khadija Kopa.
KHADIJA KOPA AJUTIA KUTOA MIMBA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment