Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kamati yake ya maudhui inafuatilia
mahojiano ya mwanamuziki Nasseb Abdul maarufu Diamond aliyoyafanya katika kituo
cha Redio cha Times jijini Dar es Salaam
Akizungumza Ofisa
Mkuu Idara ya Utangazaji ya mamlaka hiyo, Andrew Kisaka amesema wamechukua
uamuzi huo kwa kuwa mahojiano hayo yamefanyika katika kituo wanachokisimamia
Katika
mahojiano hayo, Diamond alimjibu Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na
Michezo, Juliana Shonza kutokana na Serikali kuzifungia nyimbo 15 mwezi
uliopita, zikiwemo mbili za mwanamuziki huyo
Kisaka
amefafanua kuwa kiutaratibu wao wanaangalia zaidi chombo ambacho wamekipa
leseni na kwamba, masuala mengine yatashughulikiwa na mamlaka nyingine
Amesema suala
hilo kwa sasa linafanyiwa kazi na kamati ya maudhui na kuahidi kulitolea
ufafanuzi siku za hivi karibuni akiwataka wananchi kuwa na subira
Wakati TCRA
ikisema hivyo, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison
Mwakyembe amesema amesikitishwa na matamshi ya Diamond kuhusu kufungiwa kwa
nyimbo hizo aliyoyatoa katika kipindi hicho
Diamond
amekosea kumjibu waziri
“Maamuzi ya
kuzifungia baadhi ya nyimbo za wasanii wawili kwa kukiuka maadili yalifanywa
kwa mujibu wa sheria na si kwa utashi binafsi wa Shonza ambaye analaumiwa na
Diamond,” amesema
“Diamond
atambue kuwa Serikali ina taratibu zake na maamuzi ya naibu waziri ni ya
wizara. Kama vikao na wasanii tumefanya vingi sana, lakini Diamond hakuwahi
kuhudhuria vikao hivyo, si wajibu wa Serikali kumfanyia kikao cha peke yake.”
Amesisitiza,
“Sheria ni ya watu wote bila kujali umaarufu au nafasi ya mtu katika jamii,
hivyo msanii Diamond anapaswa kutii sheria na mamlaka zilizowekwa.”
Dk Mwakyembe
ameeleza kuwa sio busara kwa Diamond kushindana na Serikali na endapo ana
ushauri wowote ni vyema akawasilisha kwa njia sahihi, lakini si kumshambulia
naibu waziri kwa dharau na kejeli kama alivyofanya
“Diamond kwa
mafanikio aliyoyapata katika muziki, anatarajiwa kuwa mfano bora kwa wanamuziki
wenzake. Napenda kuwakumbusha wasanii wote kwamba sanaa ni kazi kama zilivyo
kazi nyingine,” amesema
“Pamoja na
kuwa na kipaji hicho, wasanii wanatakiwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo
inayosimamia tasnia ya sanaa kama ilivyo kwa tasnia nyingine.”
DIAMOND AMKUNA WAZIRI MWAKYEMBE
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment