Benki kuu ya Rwanda imesema uchumi wa nchi hiyo unakadiriwa
kukua kwa asilimia 6.5 kwa mwaka huu.
Gavana wa benki ya Rwanda Bw John Rwangombwa amesema kiwango cha
mfumko wa bei kwa mwaka huu kinakadiriwa kuongezeka hadi asilimia 5
ikilinganishwa na asilimia 4.9 ya mwaka jana.
Pia amsema mwaka jana mapato yaliyotokana na uuzaji wa bidhaa
nje yaliongezeka kwa asilimia 57.6, na uagizaji wa bidhaa kutoka nje ulipungua
kwa asilimia 0.4 ikilinganishwa na mwaka 2016.
Zaidi ya hayo, aina za bidhaa
zilizouzwa nje zinaendelea kuongezeka.
Takwimu zilizotolewa na benki hiyo zinaonyesha kuwa mwaka jana
urari wa biashara ulipungua kwa asilimia 21.7 ikiliganishwa na mwaka 2016.
UCHUMI WA RWANDA WAKUA KWA ASILIMIA 6.5 KUTOKA ASILIMIA 4.9
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 07, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 07, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment