Familia ya Mwenyekiti wa
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, ambaye pia ni mwanafunzi wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) imefunguka na kuwataka watu ambao wamemteka
mwanafunzi huyo kuhakikisha anamrejesha akiwa mzima.
Baba mdogo wa Abdul Nondo amesema
hayo leo Machi 7, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari kipindi ambacho
viongozi wa mtandao huo wa wanafunzi wakitoa rai yao kwa jeshi la polisi kuhusu
kupotea kwa mwenzao.
"Abdul ni kijana mdogo mno na
amewahi kutuambia mara kwa mara kuhusu vitisho ambavyo amekuwa akivipata lakini
hatuna nguvu kusema kuwa tutamkinga vipi. Sisi kama familia tunaomba kijana
arudi akiwa mzima maana ana ndoto zake, mama yake saizi mgonjwa anaumwa
pressure baba yake pia.
Huyu Nondo ana ndoto zake kama mtoto
pia ana ndoto zake kama mwanafunzi atatimiza vipi, sisi kama familia bado
tunaendelea kulaani na tunavuta subira katika hili kwamba huenda akapatikana
tunachoomba aje salama asije akarudi hana mkono akashindwa kusonga na kumsaidia
mama yake" alisema baba
mdogo wa Abdul
Baba mdogo wa Abdul aliendelea
kusema
"Hatujui alipo lakini kama yupo
kwa wale ambao tunawasikia kila siku maanake wanajulikana tunaomba arudi huyu
kijana maisha yake na historia yake ni ngumu wamrudishe huyu kijana anatafuta
njia hana kingine anachokitafuta pale, kuongea sana vile au kujionyesha sana
vile na uwezo wa kufanya ikiwa pamoja na kusoma sana vitabu anafanya vile
kutafuta kuing'arisha ndoto yake itimie hivyo wamuache aje akamilishe ndoto
yake"
"Mama na Baba mzazi wa Abdul wana pessure baada ya mtoto wao kupotea"Familia ya Abdul Nondo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 07, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 07, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment