KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 8/3/2018 HAYA NDIYO BAADHI YA MAMBO YALIYOFANYWA NA JUMUIYA YA WANAWAKE MKOA WA ARUSHA CHINI YA MWENYEKITI YASMINI BACHU
Uongozi ni dhamana na unapopata lazima ujue unasimamia
nini na unapomtaja mwanamke kuhusu uongozi kwa siku za nyuma watu walikuwa wanapuuza
kwamba hawezi kuongoza watu bali familia yake Nyumbani.
Serikali imeweka Asilimia 50 kwa wanaume na 50 kwa
wanawake ili wanawake wapate dhamana ya kusimama kwenye uongozi na ndicho
kinachofanyika.
Tunapoelekea siku ya wanawake duniani ambayo kilele
chake ni tarehe 8 mwezi 3 mwaka 2018 tumuangazie mwanamama ambaye ni mwenyekiti
wa wanawake kwa mkoa wa Arusha Bi Yasmini Bachu ambaye alianza kazi rasmi
tarehe 6/12/2017 mpaka sasa ni miezi mitatu baada ya kupewa dhamana ya
kusimamia jumuiya ya wanawake UWT mkoa wa Arusha.
Alianza Kwa kufuatilia masuala
yote yanayohusu miradi ya jumuiya ya wanawake
ngazi ya mkoa je kwanini hawanufaiki na mali zilizopo hasa viongozi wa UWT wilayani
na wanawake wengine ndani ya mkoa wa Arusha mkoa wa Arusha unaundwa na wilaya
za kichama saba ambazo ni Monduli,Karatu,Longido,(Arumeru )Arusha Dc +Meru ,Arusha
Mjini,Ngorongoro.
Lakini safari hiyo ya kufuatilia mali za jumuiya ya Wanawake
CCM ilianza akiwa na kamati yake ya utekelezaji yawanawake ya mkoa kufuatilia mguu kwa mguu miradi hiyo ya maduka
yaliopo kata ya Kaloleni Maduka zaidi ya 72 ambayo kwa mwezi yanaingiza kiasi
sha shilingi milioni 6 tu kwa kuwa kila duka linapangishwa kwa shilingi Elfu 80
licha ya kuwa yako mjini.
Maduka yaliyopo Levolosi zaidi ya 75 ambayo kwa mwezi yanaipatia jumuiya
shilingi milioni 6 laki 5 kwa kuwa chumba kimoja kinapangishwa kwa Shilingi
Laki 1 ,ukijumlisha na maduka hayo ya kaloleni unapata Shilingi Milioni 12 na
kiasi kadhaa kwa mwezina sehemu kubwa ya fedha hizo zilikuwa zikipokelewa
mkononi ndani ya ofisi ya UWT mkoa na asilimia ndogo ndiyo zilipelekwa benki
Ikaanza safari nyingine ya kufuatilia vibanda vidogo
vidogo vya Levolosi ambavyo wafanyabiashara wanavilipia shilingi 200 bila
kujali ukubwa wake ambavyo ni zaidi ya 157 na wakati wote fedha zilikuwa
zikilipwa mkononi kwenye ofisi ya UWT Mkoa bila kutolewa risiti halali (cash
sale) utaratibu ambao fedha zote za makusanyo zilitakiwa ziingizwe benki kwa
kuwa ndiyo utaratibu wa kifedha kwa taasisi kama hii.
Tunapozungumzia uwezo wa mwanamke kiongozi tunaona
anavyotekeleza kile anachokiamini na kukisimamia kwa kuwa pia katiba ya UWT inamuongoza
vyema .Mwenyekiti Yasmini Bachu alipiga marufuku maduka hayo yaliopo kaloleni
na Levolosi kuitwa vibanda
“Katika hali ya kawaida maduka yaliyopo kaloleni yanatozwa
elfu 80 na yale ya levolosi shilingi laki 1 je ni je ni sahihi kutoza viwango
hivi kwa maeneo hayo yaliyopo katikati ya jiji la Arusha? Je Maduka
madogomadogo na mengine yaliopo nje ya halmashauri ya jiji la Arusha kama vile
Nduruma ,Bwawani Ngarenanyuki na
kadhalika yatatozwa viwango gani vya kodi ? Alihoji Yasmini Bachu
Katika Ziara hiyo Bi Yasmini Bachu pamoja na kamati yake
walishuhudia upangaji juu ya Upangaji (Maduka yamepangishiwa watu wengine
tofauti na Yule anayejulikana kwa mfano mtu x amempagishia mtu y kiasi cha
shilingi laki 3 lakini anapeleka ofisi za umoja wa wanawake Uwt Shilingi elfu
80 au laki 1) sasa je kama fedha hiyo ingekuwa inapelekwa moja kwa moja UWT
Mkoa mapato yangekuwa kiasi gani kwa Mwezi na kwa miaka kadhaa nyuma?
Baada ya ziara ya kutembelea maduka hayo na kujionea
hali halisi kamati ya utekelezaji mkoa ilifanya mkutano na kuitisha wapangaji
wote wa maeneo hayo mnamo tarehe 13/2 /2018 na kukubaliana na wapangaji hao mambo mbalimbali ikiwemo
usafi na utunzaji wa maeneo yote ya upangishaji,mikataba rasmi kuanzia tarehe
moja mwei wa 6 /2018 itakayokuwa na masharti mbalimbali ,Ongezeko la Kodi
Kuanzia tarehe moja mwezi wa 6 pamoja na pesa zote kupelekwa Bank ,madeni yote yakuanzia April hadi
December 2017 yalipwe kufikia tarehe 28 mwezi 2 2018,Maduka yote yapimwe ukubwa
na kodi mpya ilipwe kulingana na ukubwa stahili,Kuondoa kabisa suala la
upangaji juu ya upangaji na Kodi zote ziwe zikilipwa Benki kabla ya tarehe 5 ya
kila mwezi (Kwa kuwa mkataba utakuwa wa mwaka mmoja mmoja)
Hata hivyo mapato yanatazamiwa kuongezeka zaidi ya mara
mbili na nusu hadi tatu ya mapato yanayopatikana sasa hivi na jumuiya hii
imejiwekea mpango mkakati unaogusa mambo mbalimbali yatayotekelezwa kufikia
december 2018 ikiwemo kuanza kupeleka fedha kila mwezi kwenye ofisi zote za UWT
kwenye wilaya zote saba za Kichama kuanzia mwezi huu.Jambo ambalo halijawahi
kufanyika kwa miaka zaidi ya 15 iliyopita
Kutokana na hali halisi kamati ya utekelezaji mkoa
imeomba chama/Uwt Makao makuu ukaguzi maalum ufanyike kwenye miradi /mapato
yake angalau kwa miaka miwili iliyopita.
Cha kujiuliza mimi na wewe ndugu msomaji wa makala hii
inayoeleza namna kiongozi mwanamke anavyoweza kusimama katika nafasi yake na
mabadiliko chanya yakaonekana
Mwenyekiti na kamati ya utekelezaji mkoa wa Arusha
wameanza program maalum tarehe 28 mwezi wa februari ya kuwafikia makundi
makubwa ya wanawake walio na vipato vya hali ya chini kabisa wanaofanya
biashara ndogondogo za mamalishe na mbogamboga waliopo masokoni na minadani
ambao ni zaidi ya asilimia 80 ya wafanyabiashara wote wa maeneo hayo Lengo
kubwa ni kujua kero na changamoto zote wanazokutana nazo kwenye maeneo yao ya
biashara na wao kama wazalishaji wakuu na wanaotegemewa na familia
Vile vile kuona malengo ya serikali ya awamu ya tano
chini ya Mh Raisi Dokta Magufuli yanafikiwa na hasa uboreshaji wa maeneo
wanayofanyia biashara ,kuondoa ushuru usio na tija kwenye kundi hili kama
ilivyoelekezwa kwenye ilani ya CCM 2015 -2020
Pamoja na kujionea kama kundi hili wananufaika na zile
asilimia 5 zinazotengwa na halmashauri kama mikopo nafuu kwa kundi la wanawake
wajasiriamali wadogo zinawafikia program hii ni endelevu kufika masoko na
minada mbalimbali ndani ya mkoa wa Arusha.
Ndugu msomaji haya yote ni uelekeo wa uongozi mpya chini
ya Mwenyekiti wa Uwt Mkoa wa Arusha ambaye mpaka sasa ana siku 90 tu tangu alipokabidhiwa
na kupewa dhamana ya kusimamia jumuiya ya Wanawake (UWT).
Ndugu Msomaji wa makala hii kuanzia mwanzo lakini hakuna sehemu
iliyomgusa mwanaume ambaye anaaminiwa kuwa ndiye mwenye nguvu na uwezo wa
kuongoza lakini Tumemtaja mwanamke kuanzia mwanzo mpaka mwisho unapata picha
kuwa nafasi ya mwanamke katika kutumikia jamii na kusimamia nafasi yake ni
kubwa katika kuleta mabadiliko chanja .
Nikushukuru uliyetenga muda wako kusoma makala Hii
imeandaliwa na kuletwa kwako name Alphonce Saul wa Kusaganewsblog Arusha
KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 8/3/2018 HAYA NDIYO BAADHI YA MAMBO YALIYOFANYWA NA JUMUIYA YA WANAWAKE MKOA WA ARUSHA CHINI YA MWENYEKITI YASMINI BACHU
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 07, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment