Kauli Mbiu: Kuelekea Uchumi wa Viwanda tuimarishe usawa wa kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini.
Leo katika kuadhimisha Siku ya Wanawake
Duniani, Mimi kama mwanamke na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania nina kila sababu ya kuzungumza japo kwa kifupi jitihada mbalimbali
zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa na serikali katika kuimarisha
usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini.
·
Serikali inayo Sera ya
kuendeleza Wanawake, Sheria za ardhi za mwaka 1999 ambazo husimamia haki za
wanawake katika kumiliki ardhi.
·
Sera ya elimu bure inayotekelezwa
na serikali ya awamu ya tano imetoa fursa kwa watoto wengi wa kike kuandikishwa
shuleni.
·
Kuboreshwa kwa huduma za kijamii
kama vile kujengwa zahanati na vituo vya afya na usambazaji wa maji
vimempunguzia mwanamke usumbufu na hivyo kumpa muda wa kutosha kufanya shughuli
za maendeleo.
·
Usambazaji umeme vijijini
kwa kiasi kikubwa umesaidia wanawake wengi kujishughulisha na shughuli mbalimbali
za kujiingizia kipato.
·
Uwezeshaji wa Wanawake kwa
kuwapatia asilimia 5 ya mapato ya halmashauri na asilimia 30 ya zabuni za
halmashauri kumewawezesha wanawake wengi kufanya biashara na hatimaye kuwa na
uhakika wa kipato .
·
Serikali kuendelea kuhimiza
taasisi za kifedha kutoa mikopo yenye riba nafuu ili kuwawezesha wanawake wengi
kunufaika na mikopo hiyo.
·
Kurasimisha vikoba pamoja
na kuwashawishi wanawake wengi zaidi kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii ili
kuweza kunufaika na mafao na mikopo itolewayo na taasisi hizo.
Kauli Mbiu: Kuelekea Uchumi wa Viwanda tuimarishe usawa wa kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 07, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 07, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment