Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia, Dk Ave Semakafu amesema Serikali inakarabati shule za sekondari
za ufundi ili kuwaandaa wasichana kuwa wabunifu wa teknolojia ya sayansi.
Semakafu amesema hayo kwenye kongamano la
wabunifu lililoandaliwa na British Council kwa kushirikiana na Human
Development Innovation Fund (HDIF) ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kimataifa ya
wanawake duniani
Amesema kufutwa kwa shule za sekondari za
ufundi kulisababisha vijana kuanza kujifunza masuala ya ubunifu wa teknolojia
baada ya kumaliza kidato cha nne
“Vijana wanatakiwa kujifunza masuala hayo
tangu wakiwa wadogo ili waweze kuwa wabunifu na kutoa mchango wao kwa taifa,”
amesema na kuongeza serikali imeliona hilo na kuanza kuchukua hatua.
“Zipo shule nyingi zinakarabatiwa hivi sasa
ambazo ni za ufundi zitaanza kutoa elimu,” amesema.
Amesema katika mwaka wa fedha 2018/19 shule za sekondari za ufundi zitaanza kutoa elimu
“Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa wasichana
wabunifu kuanza kazi hiyo wakiwa bado na umri mdogo,” alisema
Naibu Kiongozi wa Timu wa HDIF, Joseph
Manirakiza alisema kongamano hilo limewaleta pamoja wabunifu wanawake ili
waweze kushawishi wengine kuingia katika ubunifu.
Alisema taasisi hiyo imekuwa ikisaidia
wanawake na wasichana ikiamini kwamba wanawake wakisaidiawa jamii nzima
itanufaika.
Naibu Mkuu wa Idara ya Kimataifa ya
Maendeleo ya Uingereza (DFID), Jane Miller alisema imekuwa ikisaidia wanawake
wa Tanzania katika sekta elimu, afya hasa uzazi wa mpango.
Alisema wakati huu ambao yanafanyika
maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake, Uingereza itaendelea kuwasaidia
wanawake na wasichana ili waweze kusimama wenyewe na kujitegemea
“Wanawake wanatakiwa kujiamini na kuona kuwa
wanaweza kufanya jambo lolote hata kuwazidi wanaume,” amesema.
Serikali kukarabati shule za ufundi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 07, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 07, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment