BENKI YA WANAWAKE TWB YADAI MIKOPO SUGU YENYE THAMANI YA SH BILIONI 7,6 TOKA KWA WATEJA ZAIDI YA 7000

Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) katika hatua zake za kutaka kuimarisha mtaji wake na kufanya kazi zake kwa ufanisi imewataka wateja wake 7,065 wenye mikopo sugu yenye thamani Tsh. bilioni 7.9, kulipa mikopo hiyo ndani ya siku saba vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria.


Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo, Bi. Ben Issa alisema benki imeanza kuchukua hatua za kuimarisha mtaji wake kwa kuwataka wateja wake wenye madeni sugu kulipa madeni yao ndani ya siku hizo vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa.

Moja ya mambo yanayokwamisha  kuimarika kwa mtaji na kupanua huduma za kibenki ni kuwepo kwa mikopo sugu sasa tunawataka wateja wetu wenye mikopo sugu kulipa bila shuruti vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa, aliongeza kusema,Bi Issa ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC

Alisema hatua hiyo imechukuliwa ili kuhakikisha mtaji wa benki unaimrika na itasaidia kutoa huduma za kibenki kwa ufanisi. Wakopaji wengi wamepitiliza siku 90 za urejeshaji madeni ya mikopo yao na hiyo kinyume na utaratibu wa mikataba waliyokubaliana na benki wakati wanakopa.

BENKI YA WANAWAKE TWB YADAI MIKOPO SUGU YENYE THAMANI YA SH BILIONI 7,6 TOKA KWA WATEJA ZAIDI YA 7000 BENKI YA WANAWAKE TWB YADAI MIKOPO SUGU YENYE THAMANI YA SH BILIONI 7,6 TOKA KWA WATEJA ZAIDI YA 7000 Reviewed by KUSAGANEWS on March 07, 2018 Rating: 5

No comments: