|
MEYA wa Manispaa ya Ilala jijini
Dar es Salaam, Charles Kuyeko amewataka wenyeviti wa Serikali za mitaa
wilayani humo kuacha kuwatoza fedha wananchi wanaofika katika ofisi zao kupata huduma
kwani kufanya hivyo tafsiri yake ni rushwa
|
Meya Kuyeko amesema hayo leo asubuhi alipokuwa akifungua ofisi mpya ya Serikali ya mtaa wa Mtakuja iliyopo katika kata Vingunguti Ilala jijini ambapo amesisitiza umuhimu wa viongozi wa ngazi mbalimbali kutoa huduma kwa wananchi bila kuomba fedha.
|
"Utekelezaji wa majukumu ya
ofisini, ninaomba tusiombe rushwa wananchi wanaohitaji huduma.Viongozi
endeleeni kushirikiana na wananchi ili kazi ziendelee.Nishauri wananchi
msikae na vitu moyoni, mnapaswa kupaza sauti kwa jambo lolote ili lipatiwe
ufumbuzi,"amesema Kuyeko
Kwa upande wa Diwani wa Kata ya
Vingunguti na Naibu Meya wa Manispaa hiyo , Omary Kumbilamoto amemshukuru
Meya kufanikisha ujenzi wa ofisi hiyo ambayo italeta tija kwa wananchi
waishio maeneo hayo kwani kabla ya hapo walikuwa wanatembea umbali mrefu
kufuata huduma kwa Mwenyekiti.
Aidha amemshukuru Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo kwani kupitia Wakala wa
Barabara Mijini na Vijijini( TARURA) amekubali kuifanyia matengenezo barabara
ya Vingunguti kwa Mnyamani.
Amefafanua barabara hiyo
imechimbika na hivyo kuwa na mashimo mengi kiasi cha kuifanya kutopitika kwa
urahisi na hivyo kusababisha usumbufu kwa wananchi kutokana na msongamano
mkubwa wa magari yanayosababishwa na ubovu wa barabara.
Pia amemuonya Mwenyekiti wa Mtaa
wa Mtakuja asigeuze ofisi hiyo mpya ya Serikali ya mtaa kuwa mahabusu kwa
kunyanyasa wananchi wasiokuwa na hatia,hivyo watu wote watakaokamatwa
wapelekwe kwenye vyombo vya kisheria.
|
MEYA AWAONYA WENYEVITI KUTOCHUKUA FEDHA KWA WANANCHI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 07, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment