Ratiba ya VPL yabadilika


Bodi ya ligi kuu (TPLB) imepangua ratiba ya ligi kuu soka Tanzania bara kwa mchezo mmoja kati ya Mbao FC dhidi ya Lipuli FC, uliokuwa umepangwa kuchezwa April 9 kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Mchezo huo namba 184 wa ligi, sasa umerudisha nyuma hadi April 6 na utachezwa kwenye uwanja huo huo wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Sababu za mchezo huo kurudishwa nyuma zimeelezwa kuwa ni kuipa nafasi timu ya Mbao FC kupumzika na kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Njombe Mji utakaopigwa April 11 CCM Kirumba.

Afisa mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura, tayari ameshatuma taarifa kwa klabu hizo na kuzitaka kuzingatia mabadiliko hayo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.



Ratiba ya VPL yabadilika Ratiba ya VPL yabadilika Reviewed by KUSAGANEWS on March 07, 2018 Rating: 5

No comments: