Rais wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ametuma salamu za pole kwa Chama
cha Mpira wa Miguu Cyprus kufuatia kufariki kwa aliyekuwa Rais wa FA Costakis
Koutsokoumnis akiwa na umri wa miaka 61.
Karia ametoa salamu hizo baada ya
kupokea taarifa ya kifo kilichotokea Machi 5, 2018 na kusema amesikitushwa kwa
kiasi kikubwa kwa kumpoteza mmoja wa viongozi wakongwe wa mpira wa miguu.
"Koutsokoumnis alikuwa muhimiri
mkubwa kwa soka la Cyprus na amefariki katika wakati ambao Cyprus na mpira
kiujumla ulikuwa una muhitaji, nimesikitishwa na kifo chake na ninatoa pole kwa
familia yake, FA ya Cyprus, FIFA pamoja na familia ya soka kwa ujumla", amesema Rais Karia.
Mpaka mauti yanamkuta Koutsokoumnis
alikuwa ndio Rais wa FA ya Cyprus na amekuwa kwenye kamati mbalimbali za FIFA
akiwa Makamu Mwenyekiti na alianza kutumikia soka la Cyprus tokea mwaka 1990.
Amewahi kuwa Makamu wa Rais wa FA ya Cyprus kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wa
FA mwaka 2001 nafasi aliyoitumikia mpaka mauti yanamkuta.
Raisi wa TFF Wellace Karia asikitishwa kifo cha Rais
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 07, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 07, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment