Msanii wa filamu nchini
na mmiliki wa kampuni ya RJ kwa kushirikiana na Ray, Johari amefunguka na kudai
kifo cha marehemu Steven Kanumba kimewaathiri kwa kiasi kikubwa katika utendaji
kazi wao kwa maana walikuwa wanatoa kazi kwa kushindana baina yao.
Johari amebainisha hayo wakati
alipokuwa anajibu swali kutoka kwa miongoni mwa shabiki zake aliyetaka kufahamu
kama ni kweli marehemu Steven Kanumba amekufa na bongo movie yake ?, kwa madai
kwa sasa hakuna kazi nzuri zinazofanywa kama kipindi alipokuwa hai Kanumba.
"Kuna vitu vingine vinakatisha
tamaa ila kwa upande wangu siwezi kuamini hilo kwasababu watanzania tuna
kawaida moja ya kumsifia mtu akiwa amefariki kushinda akiwa hai. Kanumba
alikuwa na mashabiki zake, nasi pia tuna mashabiki zetu 'so' siwezi kuamini
kwamba mashabiki zetu wote wamehama kutokana na mtu moja kufariki. Hiki mimi
siwezi kuamini kwamba kifo cha Kanumba kimeuwa bongo movie", amesema Johari.
Pamoja na hayo, Johari ameendelea
kwa kusema "kuondoka kwa Kanumba siwezi kusema kimeshusha au kupandisha.
Binafsi ninachokiona alipofariki Kanumba kuwa kuna baadhi ya watu wameathirika
kwa kiasi fulani au niseme sisi hapa ndio tumeaumizwa na kifo chake kwasababu
tulikuwa tunapenda ushindani wa kazi na kampuni yake".
Kwa upande mwingine, Johari ameitaka
jamii kuacha kutoa kauli zenye lengo la kuwavunja moyo kwa kuwa bongo movie ipo
hai na wasanii wapo wengi waliokuwa wazuri.
Lipa kwa M-PESA sasa na upate zawadi
na punguzo katika sehemu mbalimbali za huduma kwa kubonyeza *150*00# au MENYU
ya mtandao uliopo, VODACOM, PESA NI M-PESA
Kampuni ya RJ ,Ray na Johari kifo cha Kanumba kimetuathiri katika Utendaji wa Kazi.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 07, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 07, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment