Spika wa Bunge, Job Ndugai
anaendelea na matibabu nje ya nchi ikielezwa hali yake ya afya niaendelea vizuri ambapo yupo kwenye matibabu nje ya
nchi kwa muda sasa.
Katika mkutano wa 11 wa Bunge, hakuonekana na ilielezwa
kuwa yupo nje ya nchi kwa uchunguzi wa afya yake.
Kupitia mitandao ya kijamii
kulivumishwa habari kwamba afya ya Ndugai ambaye pia ni mbunge wa Kongwa
imedhoofu.
Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai
amesema kuwa hali ya spika
inaendelea vizuri na kwamba, anatarajia kurejea nchini wakati wowote
Ni kweli bado yuko nje ya
nchi, lakini ifahamike kuwa afya yake inaendelea vizuri na wakati wowote
atarejea nchini kuendelea na majukumu yake wala hakuna hofu kwa jambo
hilo," amesema Kagaigai.
Hata hivyo, Kagaigai hakubainisha
ni lini hasa kiongozi huyo atarejea na hakuzungumzia ugonjwa unaomsumbua wala
nchi anayotibiwa, ingawa mara nyingi amekuwa akitibiwa nchini India.
Hii ni mara ya tatu kwa Ndugai
kwenda nje kwa matibabu tangu aliposhika wadhifa wa Spika.
Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2016
ikiwa ni muda mfupi baada ya kuzinduliwa Bunge la 11.
Mara ya pili alikwenda mapema
mwaka jana, lakini kipindi hicho hakukaa muda mrefu.
Afya ya Ndugai imekuwa ikiimarika
na hata kuweza kukaa muda mrefu zaidi kwenye vikao anapokuwa Dodoma.
|
SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI KUREJEA NCHINI WAKATI WOWOTE
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 04, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment