Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,
Jaji Francis Mutungi kwa mara nyingine ametoa siku tano kwa Chama cha
demokrasia na maendeleo Chadema kujieleza kwa nini asikichukulie hatua kwa
kukiuka sheria na kanuni za maadili ya vyama vya siasa
Katika barua hiyo ya Jaji Mutungi
ya Machi mosi, 2018 iliyopokelewa Chadema Machi 2 inatakita chama hicho kikuu
cha upinzani nchini, kujieleza kwa nini kilivunja sheria na kanuni hizo
Februari 16, 2018
Barua hiyo ya Jaji Mutungi
inatokana na kutoridhishwa na majibu ya barua yake ya Februari 21
aliyokiandikia chama hicho, akikipa siku tano kujieleza kwa nini kilivunja
sheria na kanuni hizo.
Akizungumza na Mwananchi Digital
leo Machi 4, 2018, mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano na mambo ya nje wa
Chadema, John Mrema amesema barua hiyo wameipokea jana na kesho wanatarajia
kuijibu.
|
|
MSAJILI WA VYAMA ATOA SIKU 6 KWA CHADEMA KUJIELEZA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 04, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment