Na ferdinand
shayo,arusha.
Serikali mkoani
kilimanjaro itaanzisha kampeni ya kuiong'oa miti yote aina ya mikaratusi na
kuua mizizi yake ambayo inakwenda kina kirefu ardhini na kunyonya maji mengi na
hivyo kuchangia ukame na kukauka kwa vyanzo vya maji na mito
iliyoko katika hifadhi ya mlima kilimanjaro..
Mkuu wa mkoa huo bi
anna mghwira ametangaza uamuzi huo katika ibada ya maombi maalum ya kuliombea
taifa liendelee kuwa la amani na rais john magufuli kwa kazi
nzuri anayoifanya na kuyashirikisha madhehebu yote ya dini na waumini
wake yaliyoandaliwa na ofisi yake kwenye uwanja wa mashujaa mjini moshi.
Bi mghwira amesema,
miti hiyo ambayo imeota kando ya mito na vyanzo vya maji imegunduliwa kuwa ni
moja ya sababu ya kukauka kwa mito na vyanzo hivyo na amewataka
viongozi wa dini kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kuing'oa miti hiyo kwa
maelekezo yatakayotolewa na wataalam ili pia kuuhifadhi mlima k'njaro.
Askofu isaack amani wa
kanisa katoliki jimbo la moshi amewataka watanzania kuwalea watoto wao kwa
misingi ya maadili mema ili baadae taifa liwe na raia wema na viongozi
bora ambao watapambana na rushwa, ufisadi na maovu yote katika jamii ili nchi
iendelee kuwa na amani.
MITI YA MIKARATUSI KUONDOLEWA MLIMA KILIMANJARO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 04, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment