Klabu ya soka ya Azam FC
imeweka wazi kuwa haina mahusiano yoyote na timu a Al Masry, ambayo imetua
nchini leo kwaajli ya kucheza na Simba huku ikitumia Basi la klabu hiyo kutoka
Uwanja wa ndege kuelekea hotelini.
Akiongea na wanahabari msemaji
wa Azam FC Jaffary Idd Maganga amesema kuwa kutoa Basi ni sehemu ya
biashara ya klabu hivyo kwa timu yoyote ambayo inahitaji huduma hiyo ifuate tu
taratibu zote na itapata Bus.
''Basi ni sehemu ya biashara ya timu na sio mara ya kwanza
kutumika hata timu ya taifa huwa inatumia mara nyingi tu kama ilivyo kwa uwanja
wetu, na uongozi wa Simba umeandika barua kwa CEO na wamepewa lakini hatuna
mahusiano na Al Masry'', amesema.
Al Masry imetua leo nchini tayari kwa mchezo wa kwanza wa Kombe
la Shirikisho barani Afrika dhidi ya wenyeji wao Simba siku ya Jumatano Machi 7
kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Simba waazima 'Bus' la Azam FC
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 04, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment