SIKU YA TATU YA ZIARA YA MWENYEKITI UWT MKOA WA ARUSHA ASHAURI MAMBO HAYA YAFANYIKE KUSAIDIA WAFANYABIASHARA WANAWAKE

mwenyekiti wa UWT mkoa wa Arusha Yasmini Bachu akizungumza na wanawake wa soko la tengeru mkoani Arusha.
Mmoja wa akina mama wafanyabiashara wa ndizi soko la Tengeru akiwa amebeba mkungu wa ndizi kichwani kwenda kumsikiliza mwenyekiti wa Uwt mkoani baada ya kusikia amefika soko la Tengeru
Akina mama soko la Tengeru wakisikiliza anachokisema mwenyekiti Yasmini Bachu
 Mmoja wa akina mama wa biashara ya ndizi akizungumza na mwenyekiti Yasmini Mambo yanayohusu changamoto za soko la Tengeru

Mwenyekiti wa uwt Arusha Yasmini Bachu akiwa na viongozi wenzake wa wilaya ya Arumeru kwenye soko la Tengeru wakisikiliza akina mama
 Soko la Tengeru kila mtu akiwa kwenye pilika zake kufanya biashara na kununua bidhaa

Ikiwa zimesalia siku 4 kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo huadhimishwa  kila mwaka March mosi na kuishia tarehe 8 march mwenyekiti wa UWT mkoa wa Arusha Yasmini Bachu akiwa na viongozi wa UWT wilaya ya Arumeru amewatembelea akina mama wafanyabiashara katika soko la tengeru wilayani Arumeru Mkoani Arusha ili kujua changamoto wanazokutana nazo.

Akiwa ameongozana na viongozi wengine wa wilaya ya Arumeru Katika ziara yake hiyo ya siku ya tatu amesema lengo ni kuwafikia akina mama ambapo amesema asilimia 80 ya watu wanaofanya biashara masokoni ni wanawake ambao ndiyo walezi wakuu wa familia zao.

Hata hivyo amejionea mazingira katika soko hilo la Tengeru ambayo amesema siyo ya kuridhisha kutokana na kuwa maeneo ni machafu jambo ambalo ameomba mamlaka husika kutengeza maeneo rafiki ili kufanikisha biashara za akina mama zifanyike sehemu ambayo ni safi.

Bachu ameziomba halmashauri za Meru na Arusha Dc kwa kuwa alizunguka kwenye masoko hayo ikiwemo soko la Kisongo kata ya Matevez, Lokii kata ya Bwawani na Tengeru amejionea mazingira ambayo ni magumu kwa wafanyabiashara wanawake kwani masoko hayo hayana sehemu za kujisitiri endapo mvua zinanyesha

Kutokana na changamoto hizo zilizopo amezishauri halmashauri hizo kurudisha fadhila kwa wafanyabiashara ambao pia ni walipa kodi ingalau kuwatengenezea vibanda ambayo vinaweza kuwasitiri kwenye biashara zao wakati wa mvua na wakati wa Jua.

“Hapa jambo la kushauri halmashauri zetu ni kuboresha maeneo ambayo mvua ikinyesha sehemu za biashara hazipitiki na wanacha biashara zao kwenda kujikinga na mvua,upande wa vyoo pia mfano soko la kisongo choo hakiridhishi kwasababu wafanyabiashara wanaweza kupata magonjwa lakini pia na soko la Lokii hakuna choo kabisa kwasababu kuzunguka eneo hilo hakuna huduma ya choo kwakweli ni tatizo lakini najua halmashauri zetu watayatatu mapema iwezekanavyo”amesema Bachu

Nao akina mama wa soko laTengeru wamesema kuwa kuna watu wamesema kuwa changamoto walionayo katika soko hilo ni uchafu licha ya kuwa wanalipa ushuru wa taka lakini bado kuna watu wanatupa taka na asubuhi wanakuta soko ni chafu

Pia wameongeza kuwa hali ya ulinzi kwenye soko siyo nzuri kwasababu wakati mwingine wanapoacha vitu vyao vinaibiwa lakini kwa kuwa wamesema matatizo mbele ya mwenyekiti wanaamini watapata msaada mapema iwezekanavyo.


Hata hivyo mmoja wa Wazee wanawake katika soko hilo amemuomba mwenyekiti azungumze na mamlaka husika ili wapunguziwe ushuru kwasababu wameshakuwa wazee hawawezi kulipa ushuru.

Akizungumza kwa njia ya simu mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha Dc Dokta Wilson Mahera Charles amesema kuwa ameyachukua mambo hayo na atayafanyia kazi na amemshukuru mwenyekiti wa UWT kwa kuibua cchangamoto zinazowahusu wanawake hasa upande wa kuwahamasisha akina mama kukopa asilimia tano  ya fedha zinazotolewa na halmashauri zao.

“Kwakweli nimshukuru mwenyekiti nimelipata ni kitu umeniambia nitafika huko na na ni kitu very agent nitafuatilia jambo hilo mana choo ni cha msingi sana”Amesema dokta Mahera

Mahera amesema kuwa mpaka sasa kwa mwezi huu wametoa shilingi milioni 220 kwa ajili ya mikopo ya wanawake na amesema jambo ambalo anafanya mwenyekiti kuendelea kuhamasisha na kutoa elimu kuhusu mikopo hiyo.

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake mkoa wa Arusha Yasmini Bachu ameanza ziara yake ya kukutana na wanawake wafanyabiashara masokoni kutoa elimu kuhusu mikopo ya serikali na kuchukua changamoto zao na kuzifikisha sehemu husika ili zitatuliwe.


Hata hivyo kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ni “KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA TUIMARISHE USAWA WA JINSIA NA UWEZESHAJI WA WANAWAKE VIJIJINI”

SIKU YA TATU YA ZIARA YA MWENYEKITI UWT MKOA WA ARUSHA ASHAURI MAMBO HAYA YAFANYIKE KUSAIDIA WAFANYABIASHARA WANAWAKE SIKU YA TATU YA ZIARA YA MWENYEKITI UWT MKOA WA ARUSHA ASHAURI MAMBO HAYA YAFANYIKE KUSAIDIA WAFANYABIASHARA WANAWAKE Reviewed by KUSAGANEWS on March 04, 2018 Rating: 5

No comments: