Askari wa kike wa jeshi la polisi nchini Kenya anayefanya kazi
katika eneo la Kericho ameripotiwa kujipiga risasi kwa kutumia bunduki aina ya
AK 47 na kujiua kufuatia ubishani uliozuka kati yake na mpenzi wake.
Mmoja kati ya viongozi wa jeshi hilo katika eneo hilo amekiambia
kituo cha runinga cha Citizen kuwa mpenzi wa marehemu ambaye ni mfanyakazi wa
kitengo cha Hifadhi ya Wanyama Pori, alifika kwa marehemu kumtembelea lakini
walianzisha ubishani.
Ameeleza kuwa marehemu ambaye siku hiyo alikuwa katika zamu ya
usiku kazini, alienda kituoni na kuchukua bunduki aina ya AK47 na kisha
kujipiga risasi.
Mwili wake umeondolewa na jeshi la polisi na kupelekwa katika
chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya wilaya ya Kapkatet.
Chanzo cha ubishani wao bado hakijawekwa wazi, kwa mujibu wa
Citizen.
Askari polisi ajipiga risasi baada ya kubishana na mpenzi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 04, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment