Mwenyekiti wa CUF
anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Ibrahim Lipumba amesema
anaunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli
katika mpango wa ukusanyaji kodi, huku akitaka utekelezaji huo uzingatie
uhalisia
Prof. Lipumba ametoa kauli hiyo leo
wakati alivyokuwa anazungumza na waandishi wa habari baada ya ukimya wake wa
muda mrefu na kusema Baraza kuu la Chama cha Wananchi CUF linaitaka mamlaka
inayohusika na masuala ya ukusaji wa kodi kwa wafanyabiashara wawe wanatoa
makadirio mazuri ili kuweza kuwapa fursa wateja zao kulipa kodi vizuri.
"Baadhi ya makampuni na
wafanyabiashara wanakadiriwa kodi kubwa kuliko wanachouza na hatimaye biashara
zao zinafungwa. Baraza kuu la Chama cha Wananchi CUF linaitika serikali ifanye makadirio ya kodi
ambayo yatakuwa yanazingatia hali halisi, Mamlaka ya kodi isiwakamua
wafanyabiashara mpaka biashara kufungwa na kusababisha kupata
hasara", amesema Prof. Lipumba.
Pamoja na hayo, Prof. Ibrahim
Lipumba ameendelea kwa kusema "tunaunga mkono katika ukosaji wa
kodi lakini utekelezaji wake uzingatie hali halisi, tusije tukawakamua watu
wanaofanya biashara, wenye makampuni ambao wanatoa ajira mpaka biashara na
shughuli zao kupelekea kuzifunga".
Kwa upande mwingine, Prof. Lipumba
amedai Baraza kuu limepata kuwepo kwa malalamiko ya hali ya maisha kuwa magumu
kupitiliza na kuiomba serikali iongeze mzunguko wa pesa ili kuweza kuinua
maisha ya watanzania wa hali ya chini.
Prof. Lipumba amuunga mkono Rais Magufuli katika ukusanyaji wa kodi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 22, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment