Mbunge Mhe. Nape Nnauye
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii amefunguka na
kutoa ushauri wake kuhusu sekta ya utalii na kusema kuwa wanapofaya mabadiliko
yoyote lazima wame wakini wasisumbue sekta hiyo.
Nape Nnauye amesema hayo alipokuwa
akiongea na watendaji wa sekta ya utalii na kusema kuwa maboresho ambayo
wanataka kufanya ni mazuri na yenye nia ya kutaka kuleta mabadiliko lakini
lazima waangalie namna nzuri ili kutoleta shida kwenye sekta hiyo ya utalii
nchini.
"Hayo maboresho tunayofanya
yana nia njema na ni mazuri sana lakini wakati tunayatekeleza tuangalie
tusisumbue image ya Indusrty, wakati wa kufanya tuangalie sura ya tasnia
yenyewe ya utalii isisumbuliwe kwa sababu mnaweza kuwa na nia njema lakini
katika mchakato wa kufanya maboresho yenu mkajikuta mmefanya Industry yenyewe
mkaiacha hoi, naamini Waziri ni mjanja kwa sababu hawa wateja wetu ni wateja wa
shughuli za muda mrefu wakati mwingine wakiona mna maboresho yanasumbua
wakisema wanapumzika wanaweza kumpumzika jumla kwa wakati tunafanya mabadiliko,
maboresho hayo tukumbuke tuna wateja ambao ni deligents kwa sababu uamuzi wa
mtu kuja kutalii ni mtu kutenga pesa na kuamua kuja kutembea na anaweza akaamua
kwenda sehumu nyingine vilevile sababu humlazimishi aje kwako" alisema Nape Nnauye
"Nadhani wakati wa kutenda haya
mambo tusiwasumbue wateja wetu na tuwashilikishe bwana tunafanya hivi kwa faida
yenu na matokeo yake yatakuwa haya kama ni kuzuia kwa muda fulani matokeo yake
yatakuwa haya mimi nadhani tutafika salama" alisisitiza Nape Nnauye
Nape Nnauye atoa ushauri kuhusu utalii
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 22, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment