Kituo cha Redio Times cha jijini Dar
es Salaam kimetakiwa kuwasilisha kipindi cha mahojiano waliyofanya na
mwanamuziki Diamond Platinumz kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa
ajili ya uchunguzi zaidi.
Mkurugenzi wa Times FM, Amani Misana
ameieleza MCL Digital leo Machi 22, 2018 kuwa amepokea barua ya kuwataka
wawasilishe kipindi hicho kilichorushwa Machi, 19, 2018 na kwamba leo
wametekeleza agizo hilo
“Tumepokea barua na tumefanya yale
tuliyoagizwa ikiwamo kuwasilisha kipindi chote,” amesema kwa ufupi Misana.
Kaimu Meneja Mawasiliano wa TCRA,
Semu Mwakyanjala amesema suala la kituo hicho kupewa barua ni la kiutawala
zaidi na mamlaka hiyo haipo kwenye kitengo chake isipokuwa kama tayari barua
imefika, wakati wa kutolewa uamuzi vyombo vya habari vitaalikwa.
Diamond aiponza Times FM, TCRA yawalima barua
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 22, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment