Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Manendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amefunguka na kuonyesha
wasiwasi juu ya Jeshi la polisi kutaka kuwabambikizia kesi za mauaji au uhaini
ili waweze kuwekwa mahabusu muda mrefu.
Mbowe amesema hayo leo Machi 22,
2018 ikiwa ni siku ambayo yeye pamoja na viongozi wengine wa chama hicho
wanatakiwa kufika katika kituo cha polisi kusikiliza wito wa jeshi hilo na
kusema kuwa wamepata taarifa zingine kuwa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji
Peter Msigwa anataka kuhusishwa katika shauri hilo ambalo wao wanalo.
"Tuna taarifa pia ya
kusudio la kumuunganisha Mhe. Peter Msigwa, Mb, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya
Nyasa (Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa) na Mjumbe wa Kamati Kuu katika
shauri hili. Lakini pia katika wakati nenda rudi hii ikiendelea, tuna taarifa
(asante teknolojia) kuwa zinapangwa njama mahususi za kutubambikia viongozi wa
Chadema kesi za mauaji au Uhaini ili kuhalalisha azma ya Watawala kutuweka
mahabusu kwa muda mrefu, wakidhani kwa kufanya hivyo watakuwa wamefanikisha
kufifisha na hata kuua kabisa uwepo wa Upinzani katika Taifa" alisema
Mbowe
Leo Machi 22, 2018, mimi
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na viongozi wengine waandamizi wa
CHADEMA akiwepo Mhe Vincent Mashinji (Katibu Mkuu), Mhe. John John Mnyika, Mb
na Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar; Mhe
Halima J.Mdee, Mb, Mwenyekiti wa Bawacha, Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu,
Mhe.John W. Heche, Mb, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti (Mara, Simiyu
na Shinyanga) na Mjumbe wa Kamati Kuu; Mhe. Esther N. Matiko, Mb, Mwenyekiti wa
Bawacha Mkoa wa Mara na Mweka hazina wa Bawacha Taifa wanatakiwa kufika Makao
Makuu ya jeshi la polisi kwa mahojiano.
Freeman Mbowe apata wasiwasi na jeshi la Polisi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 22, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment