Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu
(AfCHPR) kesho Ijumaa Machi 23, 2018 itasoma hukumu ya kesi ya wanamuziki wa
dansi, Nguza Viking maarufu Babu Seya na mwanaye, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’
Wanamuziki hao walikata rufaa iliyosajiliwa
na kupewa namba 006/2015 katika mahakama hiyo kupinga kifungo cha maisha.
Wakati hukumu hiyo ikitarajiwa kusomwa
kesho, Babu Seya ambaye ni mtunzi wa kibao maarufu cha “Seya” na Papii Kocha
ambaye wameshirikiana katika wimbo huo ni miongoni mwa wafungwa 8,157
waliosamehewa na Rais John Magufuli siku ya Uhuru wa Tanganyika, Desemba 9,
2017
Walikuwa kati ya wafungwa 61 waliokuwa na
adhabu za vifungo vya maisha na kunyongwa ambazo si rahisi kupata msahama wa
kawaida wa mkuu wa nchi unaotolewa siku ya sherehe hizo
Rais wa mahakama hiyo, Jaji Sylvian Ore
alisema itasoma hukumu hiyo baada ya kukamilisha mahitaji yote na kupata
taarifa za wakata rufaa
Hata hivyo, wakati Jaji Ore akiahirisha
kusoma hukumu hiyo, wanamuziki hao hawakuwepo mahakamani
Baadhi ya mawakili waliokuwepo mahakamani
hapo wamesema licha ya kuwa wanamuziki hao wamepata msamaha wa rais, hukumu yao
itasomwa
"Mahakama hapa itatoa hukumu ili kuweka
rekodi za kimahakama katika kesi za aina hii na hata kama ikieleza walikuwa na
hatia haina athari kwao,” amesema wakili Daniel Kalasha
Katika kesi hiyo, Jamhuri inawakilishwa na
mawakili Sara Mwaipopo na Nkasori Sarakikya.
Hukumu ya Babu Seya, Papii Kocha kusomwa kesho
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 22, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment