Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde ameutaka Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF) kuiburuza mahakamani Shule ya Scolastica na Kampuniya
Usafirishaji ya Machare Investment kutokana na kutojisajili
katika mfuko huo.
Mavunde ametoa agizo hilo leo Machi 1, 2018
akiwa katika ziara yake ya kushtukiza na kuwabaini waajiri ambao bado
hawajatekeleza takwa lakisheria linalowataka kujisajili katika mfuko huo.
Amesema sheria ya mfuko huo
kifungu cha 71(4) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi inasema endapo mwajiri
akipatikana na hatia adhabuyake ni kulipa faini isiyozidi Sh50 milioni au
kifungo cha miakamitano jela au vyote kwa pamoja
“Serikali haitamuonea huruma mwajiri ambaye
hatafuata sheria hiyo badala yake itamburuta mahakamani,” amesema
“Serikali imeshatoa matamko mbalimbali
yanayowahimiza waajiri kutekeleza takwa hilo la kisheria na leo hii hakuna njia
nyingine, waajiri hawa tuliowabaini hapa mkoani Kilimanjaro naagiza WCF
iwapeleke mahakamani haraka iwezekanavyo ili sheria ichukue mkondo wake,”
amesema.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa mfuko huo, Anslem
Peter amesema mkoa huo una waajiri 1,039 na kwamba 525 ndio wamejisajili
huku 514 wakiwa hawajajisajili.
Mhasibu wa Shule ya Scolastica, William Mushi amesema walikuwa katika mchakato wa kujadili suala hilo na uongozi wa shule ili wawezekujisajili kwenye mfuko na kuanza kulipia.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya
Machare Invest, Henry Mosha amedai tayari wameshajaza fomu na ilibaki hatua ya
kwenda kupeleka michangoyao
NAIBU WAZIRI AAGIZA SHULE YA SCOLASTICA KUBURUZWA MAHAKAMANI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment