Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
(TMA) imesema kuanzia usiku wa leo Machi 1, 2018 hadi kesho Machi
2, 2018 kutakuwa na vipindi vya mvua kubwa katika maeneo mengi ya nyanda za
Juu Kaskazini Mashariki.
Taarifa ya TMA iliyotolewa leo
imebainisha maeneo hayo kuwa ni mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro
ambapo mvua hizo itazidi milimita 50 ndani ya saa 24 huku ilieleza hali hiyo
inatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua
TMA imewashauriwa wakazi wa maeneo
husika kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na
tahadhari zinazotolewa.
|
|
MVUA KUBWA KUANZA KESHO KANDA YA KASKAZINI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment