Mwanamke mmoja auliwa kwa kisu na watu wasiojulikana

 
Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Roda Samweli (44) Mkazi wa kijiji cha Namalandula Kata ya Namonge Wilaya ya Bukombe Mkoani  Geita ameuwa na vitu vyenye ncha kali na watu wasiojulikana huku mme wake Maziku magereja akijeruhiwa vibaya sehemu ya shingo yake, ambapo amelazwa katika hospitali ya Wilaya hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Bukombe ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama Mhe. Josephat Maganga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, huku akisema kwamba wilaya hiyo katika mwezi Febuari na Machi yametokea jumla ya matukio matatu.

Mwenyekiti   wa kijiji hicho Msindi Mbasa amesema tukio hilo limetokea juzi saa mbili  usiku ambapo watu wawili walifika nyumbani kwa Maziku Magereja na kutekeleza unyama huo, huku mtoto wa marehemu naye akisimulia namna tukio lilivyotokea.

Wakati huo huo, Mbunge wa jimbo la Bukombe ambaye ni Naibu Waziri wa madini Doto Biteko, ameitembelea familia hiyo na kuipa pole ambapo pamoja na mambo mengine amelaani vikali mauaji hayo.

Aidha Mkuu wa Wilaya Josephat Maganga amesema  Jeshi la Polisi  wilayani Bukombe  wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo  yakiwemo  na matukio mengine mawili yaliyotokea hivi karibuni.
Mwanamke mmoja auliwa kwa kisu na watu wasiojulikana Mwanamke mmoja auliwa kwa kisu na watu wasiojulikana Reviewed by KUSAGANEWS on March 05, 2018 Rating: 5

No comments: