Bannister (katikati) na Pacesetters Chris
Chataway (kulia) na Chris Brasher (kushoto) baada ya kuvunja rekodi hiyo mwaka
1954.
Sir Roger Bannister raia
wa Uingereza ambaye ni binadamu wa kwanza kukimbia maili moja chini ya dakika
nne, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88.
Bannister aliweka rekodi hiyo
ya kukimbia kwa dakika tatu na sekunde 59.4, katika uwanja wa michezo wa Iffley
Road huko Oxford Uingereza Mei 6 mwaka 1954. Wakati anavunja rekodi hiyo
alikuwa na siku 46 tu tangu ajiunge na chuo kikuu cha Oxford.
Mwanariadha huyo alikua akifanya mchezo huo kama kitu cha ziada
baada ya masomo yake ya udaktari katika Chuo Kikuu cha Oxford, lakini hiyo
haikumzuia kufikia rekodi hiyo ya juu katika mchezo wa riadha.
Bannister ambaye pia alishinda
medali ya dhahabu katika Michezo ya Jumuiya ya Madola (Commonwealth) ya mwaka
1954, amefariki kwa ugonjwa wa Parkinson ambao ulianza kumsumbua tangu mwaka
2011.
Daktari huyo aliitwa kwenye timu ya taifa ya riadha ya
Uingereza akiwa na miaka 17 na kushiriki michezo ya Olimpiki ya London ya
1948 ambapo pia alifanya vizuri.
Mtu wa kwanza kukimbia maili 1 dakika 4 afariki
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 04, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment