Shirikisho la soka
nchini Italia (IFF) limetangaza kusogeza mbele mechi zote za leo za ligi kuu
nchini humo kufuatia kifo cha beki na nahodha wa klabu ya Fiorentina David
Astori.
Klabu ya Fiorentina
imethibitisha kuwa Astori mwenye miaka 31 amekutwa kwenye chumba chake hotelini
akiwa amefariki, mapema leo ikiwa ni saa chache tu kabla ya mchezo wa ligi kuu
dhidi ya Udinese.
"Fiorentina tunasikitika kutangaza kwamba nahodha David
Astori amefariki, kwa hali hii ya kutisha na ya kushangaza, na juu ya yote
kutokana na heshima kwa familia yake tunaomba utulivu kwaajili ya taarifa
zaidi'', imeeleza taarifa ya klabu.
Baada ya muda mfupi IFF nao
wakatangaza kusogeza mbele mechi zote za leo ikiwa ni jumla ya mechi 7 zilizokuwa
zikianza kwa nyakati tofauti kama ambavyo zinaonekana kwenye picha chini.
David Astori alijiunga na Fiorentina inayoshika nafasi ya 10
kwenye msimamo, mwaka 2015 akitokea Cagliari ambayo awali ilimpeleka kwa
mkopo AS Roma na kisha Fiorentina ambayo ilimnunua moja kwa moja. Ameichezea
timu hiyo mechi 90 na kufunga mabao 3.
Msiba wasababisha mechi za leo Italia kuahirishwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 04, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment