Baada ya jana mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara kati ya
Tanzania Prison dhidi ya Mbao FC kuahirishwa dakika ya 49, kutokana na uwanja
wa Sokoine jijini Mbeya kuzidiwa na mvua, dakika 41 zilizobaki bado ni mtihani.
Dakika hizo 41 zilipangwa zichezwe
leo saa 4:00 asubuhi lakini imeshindikana kutokana na Mvua inayoendelea
kunyesha jijini Mbeya hivyo kusogezwa mbele tena.
Mchezo huo wa VPL sasa utapigwa saa
10:00 jioni kwa dakika 41 zilizosalia katika dimba hilohilo la Sokoine ambapo
pande zote mbili zimekubaliana kufanya hivyo huku pia ikisubiriwa hali ya hewa
kama itakuwa rafiki.
Wakati mchezo huo unaahirishwa
dakika ya 49 tayari wenyeji Tanzania Prison walikuwa mbele kwa bao 1-0
lilofungwa dakika ya 11 ya mchezo na Mohammed Rashid kupitia mkwaju wa Penalti.
Hadi sasa Prison ipo katika nafasi
ya tano kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 29 wakati Mbao FC ya jijini
Mwanza inashika nafasi ya 12 ikiwa na alama 19.
Mechi ya Prison na Mbao Fc yasogezwa mbele
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 04, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment