KUNDI LA AL SHABAB LAUA ASKARI POLISI WATANO KENYA



Polisi watano wameuawa nchini Kenya baada ya kushambuliwa na magaidi wa Al Shabab kutoka Somalia, wakiwa katika kambi yao katika Kaunti ya Mandera Kaskazini mwa nchi hiyo.

Shambulizi hilo lilitokea usiku wa kuamkia Ijumaa kwa mujibu wa afisa wa serikali katika Kaunti hiyo Eric Oronyi ambaye amesema, magaidi hao walivamia kambi mbili za Polisi hao katika mji wa Fino.

Aidha, Oronyi amesema magaidi hao walikuwa kati ya 70 na 100 na waliwasili katika kambi hiyo wakitembea kwa mguu.

Inaelezwa kuwa, polisi waliokuwa wanalinda malango ya kambi hizo mbili, walilemewa na kuwawezesha magaidi hao kuingia katika kambi hizo.

Mbali na mauaji hao, Polisi wengine watatu wamejeruhiwa na kusafirishwa kwenda kupata matibabu jijini Nairobi.

Magaidi hao pia wameharibu mtambo wa simu ya Safaricom kabla ya shambulizi hilo.

Kenya imeendelea kukabiliwa na tishio la Al Shabab tangu mwaka 2011, ilipotuma wanajeshi wake nchini Somalia.

KUNDI LA AL SHABAB LAUA ASKARI POLISI WATANO KENYA KUNDI LA AL SHABAB LAUA ASKARI POLISI WATANO KENYA Reviewed by KUSAGANEWS on March 05, 2018 Rating: 5

No comments: