Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewataka wafanyabiashara wa
Mkoa wa Arusha kuhakikisha wanakuwa na wataalamu wa mahesabu katika biashara
zao pamoja na kutoka risiti kila wanapofanya mauzo ili kuondokana
changamoto ya kukadiriwa ulipaji wa kodi kobwa isiyoendana na uhalisia wa mauzo
yao.
Gambo amesema hayo Leo wakati
akizindua wiki ya elimu kwa mlipa kodi Mkoa wa Arusha ambapo ameeleza
kuwa wafanya biashara wakiwa na wataalamu hao wataweza kuwasaidia kuaandaa
taarifa ya mauzo vizuri itayoonyesha uhalisia wa kodi wayopaswa kulipa pamoja
na kuondokana na ulipaji wa faini kwa kukiuka sheria ya malaka kwa
kutotoa risiti.
Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha
Faustine Mdesa ameeleza kuwa mamlaka hiyo inamkakati wa kuboresha utoaji wa
elimu kwa mlipa kodi ambapo zoezi hilo litakuwa linafanyika kila baada ya
miezi mitatu kwa lengo la kutoka nafasi ya elimu kwa upana zaidi.
Aidha katika uzinduzi huo
baadhi wa wafanyabiashara kutoka katika kundi la mabroka wa madini na wamiliki
wa migahawa wametoa changamoto zinazowakabili katika zoezi mzima za ulipaji wa
kodi ambapo wameiomba mamlaka hiyo kuweka utaratibu mzuri utakaokuwa na tija
kwako na kwa serikali.
Rc Gambo azindua wiki ya Elimu kwa Mlipa Kodi mkoa wa Arusha
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 05, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 05, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment