Chama cha Mapinduzi (CCM)
kimemkabidhi Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina
Mabula migogoro miwili ya ardhi mjini Moshi kikitaka asaidie kuipatia
ufumbuzi.
Migogoro hiyo ni pamoja na wa Pasua block
JJJ ambapo wananchi zaidi ya 100 waligawiwa viwanja na Manispaa ya Moshi
lakini kampuni ya Hodhi ya Rasilimali za Reli (Rahco), inadai ni mali yake.
Mgogoro mwingine aliouwasilishiwa
ni wa Meresini katika mji mdogo wa Himo, ambapo wananchi wananyimwa viwanja
vikiwamo vya kujenga shule, na kupewa watu wengine akiwamo mwekezaji.
Akiwasilisha migogoro hiyo jana
Februari 28, 2018 na nyaraka zake ikiwamo hati miliki kwa naibu waziri huyo,
Katibu wa CCM mkoani Kilimanjaro, Jonathan Mabhia amesema migogoro hiyo ni
kero inayohitaji majibu.
Akijibu maombi hayo, Mabula
amesema kwa kuwa mgogoro wa Pasua block JJJ umewasilishwa ukiwa na vielelezo
vya nyaraka, atazipitia nyaraka hizo na kumkabidhi kamishna wa ardhi.
Kuhusu mgogoro wa Mieresini,
amesema nalo amelichukua ili aweze kulifuatilia aone namna ugawaji huo
ulivyofanyika na kilio cha wananchi wa eneo hilo.
|
CCM yakabidhi migogoro ya ardhi kwa Mabula
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment