Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL),
imewaomba wadau, taasisi na watu wenye mapenzi mema kuiunga mkono kumchangia
mke wa mwandishi wake wa kujitegemea Azory Gwanda aliyepotea katika mazingira
ya kutatanisha.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 28,2018
ambayo Azory ametimiza siku 100 tangu atoweke, Mkurugenzi Mtendaji wa MCL,
Francis Nanai amesema Anna Pinoni ambaye ni mke wa Azory anahitaji msaada
pamoja na watoto wake wawili
“Kwa mwenye mapenzi mema ya kutusaidia atuunge mkono kwa
kuchangia kwa lipa kwa TigoPesa namba 173333 ambayo pia ni Merchant Payment
number (namba ya wakala)”
“Pesa hii itaratibiwa na MCL na itamfikia mhusika kwa
wakati, kwa ukamilifu na kwa uwazi,”amesema Nanai.
Amesema kwa yeyote anayehitaji maelezo kuhusu mchango huo
apige simu namba +255 22 5514222 aombe kuzungumza na meneja rasilimali
watu au atume maoni kupitia barua pepe
Nanai amesema MCL imeamua kusaidia kumkwamua mke wa Azory na
watoto kwa kulipia gharama za mahitaji ya watoto ya shule na kulipia huduma za
afya kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF
“Tutampatia fedha za kumwezesha kuanzisha shughuli ya
kiuchumi atakayoipenda na kuimudu na tutagharimia mahitaji mengine ya chakula
na kujikimu,”amesema Nanai.
Amesema, “Wakati Azory anatekwa mkewe alikuwa mjamzito na
tayari amejifungua mtoto wa kike aliyempa jina Gladness, tunamuomba Mungu ampe
moyo wa subira, kuvumilia upweke, mawazo na mateso ya kutomwona mwenzi na baba
wa watoto wake.”
WENYE MAPENZI MEMA WAOMBA KUJITOKEZA ILI KUSAIDIA FAMILIA YA AZORY
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 28, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 28, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment